Lengo na madhumuni ya blogu hii ni kushirikiana kutafuta na hatimaye kuwapata ndugu,jamaa na marafiki tuliopotezana nao.Kwanini uhangaike peke yako kumtafuta nduguyo mliyepoteana kitambo ilhali tunaweza kushirikiana kumtafuta?Waswahili wana msemo kuwa kidole kimoja hakivunji chawa.Naam,japo yawezekana kabisa kuwa jitihada zako peke yako zinaweza kukusaidia kumpata unayemtafuta,ushiriki wa wengi kumtafuta mtu huyo unaweza kurahisisha kazi hiyo.
Kwahiyo basi,kama ulipotezana na ndugu,jamaa au rafiki,au mtu yeyote yule,cha kufanya ni kukutumia jina lake kamili,mahali mlipokuwa pamoja au/ma mlipopoteana (kwa mfano shuleni,kambi ya JKT,chuoni,nk) na jinsi anavyoweza kuwasiliana nawe.Ukiwa na picha ya unayemtafuta itakuwa bora zaidi lakini cha muhimu zaidi ni jina lako na lake.Kwa kutumia mahusiano yetu mazuri na vyombo mbalimbali vya habari tutasambaza tangazo hilo ili liwafikie watu wengi zaidi tukitarajia mlengwa anayetafutwa atakuwa miongoni mwa watakaosoma tangazo hilo.
Huduma hii ni ya bure kabisa,na lengo ni kudumisha utamaduni wetu wa Kiafrika wa kusaidiana katika kila jambo.
Karibuni sana kuTAFUTA na hatimaye kuPATA
No comments:
Post a Comment